Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 44:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 44:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?


Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?


Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee BWANA, milele na milele.


Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA Pasaka, wanaume wake wote watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya Pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle.


kuwa mmewaingiza wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu pangu, wapatie unajisi, naam, nyumba yangu, mtoapo sadaka ya chakula changu, mafuta na damu; nao wameyavunja maagano yangu, juu ya machukizo yenu yote.


Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.


mimi nami nimewaendea kinyume, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao;


Naam, kila chombo katika Yerusalemu, na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa BWANA wa majeshi; nao wote watoao dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya nyumba ya BWANA wa majeshi.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize.


Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo