Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 43:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Na huo utukufu wa BWANA ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nao utukufu wa Mwenyezi-Mungu uliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya lango la mashariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nao utukufu wa Mwenyezi-Mungu uliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya lango la mashariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nao utukufu wa Mwenyezi-Mungu uliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwa njia ya lango la mashariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaingia hekaluni kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Utukufu wa bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 43:4
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.


Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.


Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.


Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.


Utukufu wa BWANA ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji.


Ndipo roho ikaniinua, nami nikasikia nyuma yangu sauti kama mshindo wa radi kuu, ikisema, Na uhimidiwe utukufu wa BWANA tokea mahali pake.


Kisha akanileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki;


na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.


BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa.


Kisha akanileta, kwa njia ya lango la upande wa kaskazini, mbele ya nyumba; nikaangalia, na tazama, huo utukufu wa BWANA uliijaza nyumba ya BWANA; nikaanguka kifudifudi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo