Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 42:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Baada ya yule mtu kulipima eneo la ndani la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alinitoa nje kupitia lango la mashariki na kulipima eneo la nje.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Baada ya yule mtu kulipima eneo la ndani la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alinitoa nje kupitia lango la mashariki na kulipima eneo la nje.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Baada ya yule mtu kulipima eneo la ndani la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alinitoa nje kupitia lango la mashariki na kulipima eneo la nje.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka:

Tazama sura Nakili

Ezekieli 42:15
7 Marejeleo ya Msalaba  

Tena akatengeneza ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake.

Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.

Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia moja; na hekalu la ndani, na kumbi za ua;

Kisha akanileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki;

Katika hiyo itakuwako sehemu kwa mahali patakatifu, urefu wake mia tano, na upana wake mia tano, mraba pande zote; na dhiraa ishirini kwa viunga vyake pande zote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo