Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 41:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Basi akaipima nyumba, urefu wake dhiraa mia moja; na mahali pale palipotengeka na jengo lile, pamoja na kuta zake, urefu wake dhiraa mia moja;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Yule mtu akapima upande wa nje wa hekalu nao ulikuwa na urefu wa mita 50. Tokea nyuma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kupitia ile nafasi ya kupitia, hadi mwisho wake, upande wa magharibi, umbali wake ulikuwa pia mita 50.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Yule mtu akapima upande wa nje wa hekalu nao ulikuwa na urefu wa mita 50. Tokea nyuma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kupitia ile nafasi ya kupitia, hadi mwisho wake, upande wa magharibi, umbali wake ulikuwa pia mita 50.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Yule mtu akapima upande wa nje wa hekalu nao ulikuwa na urefu wa mita 50. Tokea nyuma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kupitia ile nafasi ya kupitia, hadi mwisho wake, upande wa magharibi, umbali wake ulikuwa pia mita 50.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kisha akapima Hekalu; lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kisha akapima Hekalu, lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 41:13
8 Marejeleo ya Msalaba  

Akaupima huo ua, na urefu wake ulikuwa dhiraa mia moja, na upana wake dhiraa mia moja, mraba; nayo madhabahu yalikuwa mbele ya nyumba.

Nalo jengo lililokabili mahali palipotengeka upande wa magharibi, upana wake dhiraa sabini; na ukuta wa lile jengo, unene wake dhiraa tano pande zote, na urefu wake dhiraa tisini.

tena upana wa uso wa nyumba, na wa mahali palipotengeka upande wa mashariki, dhiraa mia.

Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia moja; na hekalu la ndani, na kumbi za ua;

Ndipo akanileta mpaka ua wa nje, njia ya kuelekea upande wa kaskazini; akaniingiza katika chumba kilichopakabili mahali palipotengeka, na kilicholikabili jengo upande wa kaskazini;

Tena palikuwa na vyumba katika unene wa ukuta wa ua, kuukabili upande wa mashariki, kupaelekea mahali palipotengeka, na kulielekea jengo.

kukabili urefu wa dhiraa mia moja palikuwa na mlango wa kaskazini, na upana wake ni dhiraa hamsini.

Maana urefu wa vyumba vile, vilivyokuwa katika ua wa nje, ulikuwa dhiraa hamsini; na tazama, mbele ya hekalu, dhiraa mia moja.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo