Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 4:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Nawe utauelekeza uso wako, uelekee kuzingirwa kwa Yerusalemu, na mkono wako utakuwa haukuvikwa nguo, nawe utatoa unabii juu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 “Kisha, utauelekea mji wa Yerusalemu uliozingirwa na kuunyoshea mkono mtupu na kutabiri dhidi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 “Kisha, utauelekea mji wa Yerusalemu uliozingirwa na kuunyoshea mkono mtupu na kutabiri dhidi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 “Kisha, utauelekea mji wa Yerusalemu uliozingirwa na kuunyoshea mkono mtupu na kutabiri dhidi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Geuza uso wako uuelekeze Yerusalemu uone jinsi ulivyozingirwa, na kwa mkono wako usiovikwa nguo, tabiri dhidi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Geuza uso wako uelekeze kwenye kuzingirwa kwa Yerusalemu na mkono wako ambao haukuvikwa nguo tabiri dhidi yake.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 4:7
6 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.


Mwanadamu, uelekeze uso wako Yerusalemu, ukadondoze neno lako upande wa mahali patakatifu, ukatabiri juu ya nchi ya Israeli;


Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati ya wewe na mji huo; ukaelekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.


Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za kuzingirwa zitakapomalizika; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.


Mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame milima ya Israeli, ukaitabirie,


Naye atakaza uso wake ili aje pamoja na nguvu zote za ufalme wake, naye atafanya mapatano naye; naye atatenda kadiri apendavyo; naye atampa binti amuoe, ili hatimaye amwangamize huyo mfalme; lakini hataweza kumwangamiza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo