Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 38:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 38:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.


Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; hauchukii ubaya.


Mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye.


Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.


Mna upotovu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.


Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;


Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.


Roho ya BWANA ikaniangukia, naye akaniambia, Nena, BWANA asema hivi; Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu.


Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.


Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,


Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;


Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuhifadhi kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?


Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.


Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.


Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo