Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 36:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote, waliojiandalia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa ujeuri wa roho zao, wakatwaa nchi yangu kuwa milki yao, kwa sababu ya malisho yake, ili kuipora;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’

Tazama sura Nakili




Ezekieli 36:5
32 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!


Ee BWANA, hadi lini? Utaona hasira milele? Wivu wako utawaka kama moto?


Amchekaye maskini humtukana Muumba wake; Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.


BWANA asema hivi juu ya jirani zangu wote walio wabaya, waugusao urithi wangu niliowarithisha watu wangu Israeli, Tazama, nitawang'oa katika nchi yao, nami nitaing'oa nyumba ya Yuda isiwe kati yao.


angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.


Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?


Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;


Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi.


basi tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu, naam, kwa sababu wamewafanya ninyi kuwa ukiwa, na kuwameza pande zote, mpate kuwa milki kwa mabaki ya mataifa, nanyi mmesemwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu;


basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmetukanwa na mataifa;


Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;


Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.


Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.


Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.


Basi ningojeeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.


Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Haya, piga kelele na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Naona wivu kwa ajili ya Yerusalemu, na kwa ajili ya Sayuni; naona wivu mkuu sana.


Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.


na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.


kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto uangamizao, Mungu mwenye wivu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo