Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 35:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Hivyo ndivyo nitakavyoufanya mlima Seiri kuwa ajabu na ukiwa; nami nitakatilia mbali nao mtu apitaye, na mtu arejeaye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nitaufanya mlima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote apitaye huko nitamwangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nitaufanya mlima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote apitaye huko nitamwangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nitaufanya mlima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote apitaye huko nitamwangamiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaoenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 35:7
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.


Hautapita kati yake mguu wa mwanadamu, wala hautapita kati yake mguu wa mnyama, wala haitakaliwa na watu, muda wa miaka arubaini.


Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, na kiburi cha uwezo wake kitakoma; nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa, asipite mtu.


uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu.


Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitakuweka tayari kwa damu, na damu itakufuatia; ikiwa hukuchukia damu, basi damu itakufuatia.


Nami nitaijaza milima yake watu wake waliouawa; katika milima yako, na katika mabonde yako, na mito yako yote, wataanguka wao watakaouawa kwa upanga.


Nitakufanya kuwa ukiwa wa daima, na miji yako haitakaliwa na watu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo