Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 35:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 kama wewe ulivyofanya wakati nchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mlima Seiri, pamoja na nchi yote ya Edomu. Ndipo watu watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 kama wewe ulivyofanya wakati nchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mlima Seiri, pamoja na nchi yote ya Edomu. Ndipo watu watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 kama wewe ulivyofanya wakati nchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mlima Seiri, pamoja na nchi yote ya Edomu. Ndipo watu watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee Mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi bwana.’ ”

Tazama sura Nakili




Ezekieli 35:15
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!


Amchekaye maskini humtukana Muumba wake; Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.


Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;


Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi.


Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako;


Edomu yuko huko, wafalme wake, na wakuu wake wote, ambao katika uwezo wao wamelazwa pamoja nao waliouawa kwa upanga; watalala pamoja na hao wasiotahiriwa, na pamoja na hao washukao shimoni.


Nitakufanya kuwa ukiwa wa daima, na miji yako haitakaliwa na watu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli, useme, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la BWANA.


Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.


Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.


Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.


na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo