Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 34:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Na ninyi, kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 “Nyinyi, kundi la kondoo wangu, ni nyinyi watu wangu, nami ni Mungu wenu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 “Nyinyi, kundi la kondoo wangu, ni nyinyi watu wangu, nami ni Mungu wenu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 “Nyinyi, kundi la kondoo wangu, ni nyinyi watu wangu, nami ni Mungu wenu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu; ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema bwana Mwenyezi.’ ”

Tazama sura Nakili




Ezekieli 34:31
16 Marejeleo ya Msalaba  

Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.


Kisha akawaongoza watu wake kama kondoo, Akawachunga kama kundi jangwani.


Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.


Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!


Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.


Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.


Tena neno la BWANA likanijia, kusema,


Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu, miji ile iliyokuwa maganjo; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.


Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.


Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.


Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.


Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo