Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 33:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Hivi ndivyo utakavyowaambia, Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika watu wale wakaao mahali palipoharibika wataanguka kwa upanga, naye mtu aliye katika uwanda, nitamtoa na kuwapa wanyama wakali, ili aliwe; na hao walio ndani ya ngome na mapango watakufa kwa tauni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Waambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Waambie hivi: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 33:27
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.


Basi, shimo lile, ambalo Ishmaeli amezitupa maiti za watu aliowaua, karibu na Gedalia, (ni lile lile alilolichimba Asa, mfalme, kwa kuwa alimwogopa Baasha, mfalme wa Israeli), Ishmaeli, mwana wa Nethania, akalijaza kwa watu wale aliowaua.


Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.


Nami nitawatwaa mabaki wa Yuda, walioelekeza nyuso zao kuiingia nchi ya Misri, wakae huko, nao wataangamia wote pia; wataanguka katika nchi ya Misri; wataangamia kwa upanga, na kwa njaa; watakufa, tangu wadogo hata wakubwa, kwa upanga, na kwa njaa; nao watakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu.


Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?


Mwanadamu, watu wale wakaao mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli husema ya kwamba, Abrahamu alikuwa mmoja, akairithi nchi hii; lakini sisi tu watu wengi; tumepewa nchi hii iwe urithi wetu.


Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa pori, uliwe na wao.


Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA.


Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome.


Hata Waisraeli walipoona ya kuwa wako katika dhiki, (maana watu walifadhaishwa), ndipo hao watu wakajificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika.


Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko.


Basi Daudi alikuwa akikaa nyikani ngomeni, akakaa katika nchi ya milima milima kwenye nyika ya Zifu. Naye Sauli alikuwa akimtafuta kila siku, lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.


Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo