Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 33:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Japo ninapomwambia mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akitenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika ataishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa; atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 33:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.


Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.


Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.


Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.


Mwenye haki ageukapo, na kuiacha haki yake, na kutenda maovu, atakufa katika maovu hayo.


Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.


tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;


Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.


Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo