Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 32:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Nami nitakuacha juu ya nchi kavu, nitakutupa juu ya uso wa uwanda, nami nitawaleta ndege wote wa angani watue juu yako, nami nitawashibisha wanyama wa dunia yote kwako wewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nitakutupa juu ya nchi kavu, nitakubwaga uwanjani, nitawafanya ndege wote watue juu yako, na kuwashibisha wanyama wote wa porini kwa mwili wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nitakutupa juu ya nchi kavu, nitakubwaga uwanjani, nitawafanya ndege wote watue juu yako, na kuwashibisha wanyama wote wa porini kwa mwili wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nitakutupa juu ya nchi kavu, nitakubwaga uwanjani, nitawafanya ndege wote watue juu yako, na kuwashibisha wanyama wote wa porini kwa mwili wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Nitakutupa nchi kavu na kukuvurumisha uwanjani. Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako na wanyama wote wa nchi watajishibisha nyama yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Nitakutupa nchi kavu na kukuvurumisha uwanjani. Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako na wanyama wote wa nchi watajishibisha nyama yako.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 32:4
19 Marejeleo ya Msalaba  

Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwamwitu.


Wewe ulivivunja vichwa vya Lewiathani, Awe chakula cha watu wa jangwani.


Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.


Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na wanyama wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na wanyama wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi.


Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.


Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.


nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.


Nami nitakuacha ukiwa umetupwa jangwani, wewe na samaki wote wa mito yako; utaanguka katika uwanda ulio wazi; hutakusanywa, wala kuwekwa pamoja; nimekutoa uwe chakula cha wanyama wa nchi, na cha ndege wa angani.


Nami nitaijaza milima yake watu wake waliouawa; katika milima yako, na katika mabonde yako, na mito yako yote, wataanguka wao watakaouawa kwa upanga.


Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo