Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 32:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Kwa panga za mashujaa nitawaangusha watu wako umati wote; hao wote ni watu wa mataifa watishao, nao watakiharibu kiburi cha Misri, na jamii ya watu wake wengi wataangamia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Nitayafanya makundi yako kuanguka kwa panga za mashujaa: taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote yatashindwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka kwa panga za watu mashujaa, taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote ya wajeuri yatashindwa.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 32:12
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.


Wote wakujuao kati ya makabila ya watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.


basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.


Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake.


Yeye, na watu wake pamoja naye, watu wa mataifa watishao, wataletwa waingie katika nchi waiharibu, nao watafuta panga zao wapigane na Misri, na kuijaza nchi wale waliouawa.


mimi nitamtia katika mikono yake aliye mkuu kati ya mataifa; naye atamtenda mambo; nimemfukuza kwa sababu ya uovu wake.


Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.


Mwanadamu, walilie watu wa Misri. Wote jamii ukawabwage, naam, yeye, na binti za mataifa mashuhuri, hata pande za chini za nchi, pamoja na watu washukao shimoni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo