Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Ezekieli 31:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Hao nao waliteremka kuzimuni pamoja naye kwa watu waliouawa kwa upanga; naam, wale waliowasaidia, waliokaa chini ya uvuli wake kati ya mataifa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Hiyo nayo ilishuka huko kuzimu pamoja nao, ikajiunga na wale waliofungamana nao na ambao waliburudika chini ya kivuli chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Hiyo nayo ilishuka huko kuzimu pamoja nao, ikajiunga na wale waliofungamana nao na ambao waliburudika chini ya kivuli chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Hiyo nayo ilishuka huko kuzimu pamoja nao, ikajiunga na wale waliofungamana nao na ambao waliburudika chini ya kivuli chake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 31:17
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.

Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.

Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.

Tazama, Mwashuri alikuwa mwerezi katika Lebanoni, wenye matawi mazuri, na kifuniko chenye uvuli, na kimo kirefu; na kilele chake kilikuwa kati ya matawi mapana.

Ndege wote wa angani walifanya viota vyao katika vitanzu vyake, na chini ya matawi yake wanyama wote wa kondeni walizaa watoto wao, na chini ya uvuli wake mataifa makuu yote walikaa.

lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo