Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 31:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Basi Bwana MUNGU asema hivi; kwa kuwa umetukuzwa kimo chako, naye ameweka kilele chake kati ya mawingu, na moyo wake umeinuka kwa urefu wake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 “Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa sababu wewe ulirefusha kimo chake na kukiinua kilele chake kati ya matawi makubwa, ukajivunia urefu wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 “Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa sababu wewe ulirefusha kimo chake na kukiinua kilele chake kati ya matawi makubwa, ukajivunia urefu wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 “Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa sababu wewe ulirefusha kimo chake na kukiinua kilele chake kati ya matawi makubwa, ukajivunia urefu wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake,

Tazama sura Nakili




Ezekieli 31:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wasema, Tazama, umewapiga Edomu; na moyo wako wakutukuza ujisifu; kaa nyumbani mwako basi; mbona unataka kujitia bure katika madhara, hata uanguke, wewe na Yuda pamoja nawe?


Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.


Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.


Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.


Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.


Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.


ili mti wowote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.


Tazama, Mwashuri alikuwa mwerezi katika Lebanoni, wenye matawi mazuri, na kifuniko chenye uvuli, na kimo kirefu; na kilele chake kilikuwa kati ya matawi mapana.


Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.


Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?


Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, alishushwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.


Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?


Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.


Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo