Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Kushi, na Putu, na Ludi, na watu wote waliochanganyika, na Kubu, na wana wa nchi ya agano, wataanguka kwa upanga pamoja nao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Watu wote waliofungamana na Wamisri, yaani watu wa Kushi, Puti, Ludi, Arabia yote na Libia wataangamia pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Watu wote waliofungamana na Wamisri, yaani watu wa Kushi, Puti, Ludi, Arabia yote na Libia wataangamia pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Watu wote waliofungamana na Wamisri, yaani watu wa Kushi, Puti, Ludi, Arabia yote na Libia wataangamia pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Kubu na watu wa nchi ya agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:5
13 Marejeleo ya Msalaba  

akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.


Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;


vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.


na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;


na wafalme wote wa Arabuni, na wafalme wote wa watu waliochanganyika wakaao jangwani;


Tazama, nawaangalia niwaletee mabaya, wala si mema; nao watu wote wa Yuda, walioko hapa katika nchi ya Misri, wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa, hadi wakomeshwe kabisa.


Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.


Upanga uko juu ya farasi wao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa.


Watu wa Uajemi na Ludi na Putu walikuwa katika jeshi lako, watu wako wa vita; walitungika ngao na chapeo ndani yako; wakadhihirisha uzuri wako.


Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;


Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake.


Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo