Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Na upanga utakuja juu ya Misri, na dhiki itakuwa katika Kushi, watakapoanguka watu waliouawa katika Misri, nao watauondoa wingi wa watu wake, na misingi yake itabomolewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Kushi. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:4
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu hiyo Moabu atalia kwa ajili ya Moabu, kila mmoja atalia, maana mtaiombolezea mikate ya zabibu ya Kir-Haresethi, mkipigwa sana.


Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;


Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.


Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake ikiwa haina viatu. BWANA akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, bila viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi;


Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.


Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.


Maana nitampelekea tauni, na damu, katika njia kuu zake, na hao waliotiwa jeraha wataanguka kati yake, kwa upanga juu yake pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arubaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.


Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake.


Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitaleta upanga juu yako, nami nitakatilia mbali nawe wanadamu na wanyama.


Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;


Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake.


Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo