Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Kwa maana siku ile i karibu, siku ile ya BWANA i karibu, siku ya mawingu; itakuwa wakati wa maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kwa maana, siku hiyo imekaribia; siku ile ya Mwenyezi-Mungu iko karibu. Hiyo itakuwa siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kwa maana, siku hiyo imekaribia; siku ile ya Mwenyezi-Mungu iko karibu. Hiyo itakuwa siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kwa maana, siku hiyo imekaribia; siku ile ya Mwenyezi-Mungu iko karibu. Hiyo itakuwa siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Mwenyezi Mungu imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:3
35 Marejeleo ya Msalaba  

Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Atawaponda wakuu katika nchi nyingi.


BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.


ikawa katikati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha.


Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri.


Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.


Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.


Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.


Mshindo utafika hata mwisho wa dunia; Maana BWANA ana mashindano na mataifa, Atateta na watu wote wenye mwili; Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema BWANA.


Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa, wala hamkuitengenezea nyumba ya Israeli boma, wapate kusimama vitani katika siku ya BWANA.


Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arubaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.


Huko Tapanesi nako mchana utakuwa giza, nitakapovunja huko kongwa za Misri, na kiburi cha uwezo wake kitakoma ndani yake, na katika habari zake, wingu litaifunika, na binti zake watakwenda utumwani.


Nami nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu, wala mwezi hautatoa nuru yake.


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Angalia, siku hiyo; angalia, inakuja; ajali yako imetokea; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka.


Majira yamewadia, siku ile inakaribia; huyo anunuaye asifurahi, wala asihuzunike auzaye; maana ghadhabu imewapata watu wote.


Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya BWANA; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.


Ajali yako imekujia, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.


Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.


Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.


Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!


Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya BWANA iko karibu; Kwa kuwa BWANA ametayarisha dhabihu, Amewatakasa wageni wake.


nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yote, tambueni ya kuwa yuko karibu, katika malango.


Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu.


Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kuistahimili?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo