Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Nami nitaitegemeza mikono ya mfalme wa Babeli, na mikono ya Farao itaanguka; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoutia upanga wangu katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye ataunyosha juu ya nchi ya Misri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Mikono ya mfalme wa Babuloni nitaiimarisha, lakini mikono ya Farao italegea. Hapo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Nitakapotia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babuloni, ataunyosha dhidi ya nchi ya Misri,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Mikono ya mfalme wa Babuloni nitaiimarisha, lakini mikono ya Farao italegea. Hapo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Nitakapotia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babuloni, ataunyosha dhidi ya nchi ya Misri,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Mikono ya mfalme wa Babuloni nitaiimarisha, lakini mikono ya Farao italegea. Hapo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Nitakapotia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babuloni, ataunyosha dhidi ya nchi ya Misri,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi bwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:25
13 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia.


BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.


Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Wala hautakuwa tena tegemeo la nyumba ya Israeli, kufanya maovu yakumbukwe, watakapogeuka kuangalia nyuma yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.


Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe, nami nitakujalia kufumbua kinywa kati yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Hivyo ndivyo nitakavyotekeleza hukumu katika Misri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nami nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, na kuutia upanga wangu katika mkono wake, bali mikono ya Farao nitaivunja, naye ataugua mbele yake, kwa mauguzi ya mtu aliyetiwa jeraha la kumwua.


Nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, na kuwatapanya kati ya nchi mbalimbali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nitakapoifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa na jangwa, nchi iliyopungukiwa na vitu vilivyoijaza, nitakapowapiga watu wote wakaao ndani yake, ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


nawe utapanda juu uwajie watu wangu, Israeli, kama wingu likiifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kupitia kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.


Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Haya, unyoshe huo mkuki ulio nao mkononi mwako, uuelekeze upande wa Ai; kwa kuwa nitautia mkononi mwako. Basi Yoshua akaunyosha huo mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea huo mji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo