Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Nami nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa, nami nitatia moto katika Soani, nami nitatekeleza hukumu katika No.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mji wa Pathrosi nitaufanya kuwa mtupu, mji wa Soani nitauwasha moto, mji wa Thebesi nitauadhibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mji wa Pathrosi nitaufanya kuwa mtupu, mji wa Soani nitauwasha moto, mji wa Thebesi nitauadhibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mji wa Pathrosi nitaufanya kuwa mtupu, mji wa Soani nitauwasha moto, mji wa Thebesi nitauadhibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga Thebesi kwa adhabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:14
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu, Katika nchi ya Misri, konde la Soani.


Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika uwanda wa Soani.


Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.


Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?


Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameipotosha Misri.


Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi.


Neno lililomjia Yeremia, kuhusu Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tapanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema,


Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema,


BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;


nami nitawarejesha Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha Pathrosi, nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni.


Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake.


Nami nitamwaga ghadhabu yangu juu ya Sini, ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali wingi wa watu wa No.


Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.


Hivyo ndivyo nitakavyotekeleza hukumu katika Misri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoweka moto katika Misri, na hao wote wamsaidiao watakapoangamia.


Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake.


Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo