Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 30:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi. Hapatakuwa tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 30:13
18 Marejeleo ya Msalaba  

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.


Nazo sanamu zitatoweka kabisa.


Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.


Tena wana wa Nofu na Tapanesi wamevunja utosi wa kichwa chako.


Nami nitawasha moto katika nyumba za miungu ya Misri, na kuziteketeza, na kuwachukua mateka; naye atajipamba kwa nchi ya Misri, kama vile mchungaji avaavyo nguo zake; naye atatoka huko na amani.


Naye atazivunja nguzo za Beth-shemeshi, iliyoko huko katika nchi ya Misri, na nyumba za miungu ya Misri ataziteketeza.


Neno lililomjia Yeremia, kuhusu Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tapanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema,


Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.


Ee binti ukaaye katika Misri, Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa; Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa, Utateketezwa, usikaliwe na watu.


BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;


Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.


Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.


Kwa maana, tazama, wamekwenda zao ili kukimbia uharibifu, lakini Misri itawakusanya, Nofu itawazika; vitu vyao vya fedha viwapendezavyo, magugu yatavimiliki; miiba itakuwa katika hema zao.


BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.


Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.


Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo