Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 27:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Walichukua mialoni kutoka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 27:6
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.


Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani;


Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari.


Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hadi Kitimu; huko nako hutapata raha.


Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wowote.


Haya panda Lebanoni, ukalie Upalize sauti yako katika Bashani; Ukalie kutoka Abarimu; Maana wapenzi wako wote wameangamia.


Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhibikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.


Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.


Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote.


Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atapata uharibifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo