Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 26:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Nao watakufanyia maombolezo, na kukuambia, Imekuwaje wewe kuharibika, wewe uliyekaliwa na wanamaji, mji wenye sifa, uliyekuwa na nguvu katika bahari, mji huo, na hao waliokaa ndani yake, waliowatia hofu wote waliokaa ndani yake!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Wataimba utenzi huu wa kuomboleza: Umeangamizwa wewe mji maarufu, umetoweka kutoka baharini! Wakazi wake walieneza nguvu zao juu ya bahari, ambapo walihofiwa na wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, ee mji uliokuwa na sifa, wewe uliyekaliwa na mabaharia! Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, wewe na wakaaji wako; wote walioishi huko, uliwatia hofu kuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, ee mji uliokuwa na sifa, wewe uliyekaliwa na mabaharia! Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, wewe na watu wako; wote walioishi huko, uliwatia hofu kuu.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 26:17
27 Marejeleo ya Msalaba  

Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka!


Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!


Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona uchungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali.


Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?


Jinsi alivyovunjika! Ombolezeni! Jinsi Moabu alivyogeuza kisogo kwa haya! Hivyo ndivyo Moabu atakavyokuwa dhihaka, na sababu ya kuwashangaza watu wote wamzungukao.


Imekuwaje nyundo ya dunia yote Kukatiliwa mbali na kuvunjwa? Imekuwaje Babeli kuwa ukiwa Katikati ya mataifa?


Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.


Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana BWANA amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.


Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.


Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!


Tena uwaombolezee wakuu wa Israeli,


Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.


Hayo ndiyo maombolezo watakayoimba; binti za mataifa watayaimba; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake umati wote, asema Bwana MUNGU.


Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.


ambao makaburi yao yamewekwa pande za shimo zilizo mbali sana, umati wote wamezunguka kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, waliotisha katika nchi yao walio hai.


Je! Wasilale pamoja na mashujaa wao wasiotahiriwa, walioanguka, walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita, ambao wameweka panga zao chini ya vichwa vyao, na maovu yao mifupani mwao? Maana waliwatisha mashujaa katika nchi ya walio hai.


Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.


Kama wezi wangekujia, kama wanyang'anyi wangekujia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?


Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema, Sisi tumeangamizwa kabisa; Yeye analibadili fungu la watu wangu; Jinsi anavyoniondolea hilo! Awagawia waasi mashamba yetu.


Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa salama, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.


kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo