Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 23:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

40 Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kuremba kwa mapambo mazuri;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 “Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 “Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 “Hata walituma wajumbe wawaite watu wa mbali, nao wakaja. Kwa ajili yao, walioga, wakajitia wanja na kujipamba kwa johari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 “Hata waliwatuma wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako wanja, na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 “Walituma hata wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako rangi na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 23:40
13 Marejeleo ya Msalaba  

Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.


Basi zamu ya kila mwanamwali kuingia kwa mfalme Ahasuero, iliwadia baada ya kutayarishwa kulingana na sheria ya wanawake kwa miezi kumi na miwili; kwa kuwa ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;


Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.


Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;


Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hadi kuzimu.


Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.


Nikaona ya kuwa ametiwa unajisi; wote wawili walifuata njia moja.


Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.


Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;


Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; lakini usijioneshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo