Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 23:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Bwana MUNGU asema hivi; Utakinywea kikombe cha dada yako; chenye kina kirefu na kipana; utadhihakiwa na kudharauliwa; nacho kimejaa sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Utakunywa toka kikombe cha dada yako; kikombe kikubwa na cha kina kirefu. Watu watakucheka na kukudharau; na kikombe chenyewe kimejaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Utakunywa toka kikombe cha dada yako; kikombe kikubwa na cha kina kirefu. Watu watakucheka na kukudharau; na kikombe chenyewe kimejaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Utakunywa toka kikombe cha dada yako; kikombe kikubwa na cha kina kirefu. Watu watakucheka na kukudharau; na kikombe chenyewe kimejaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; kitakuletea dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 “Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; nitaletea juu yako dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 23:32
23 Marejeleo ya Msalaba  

basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.


Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.


Umewaonesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.


Wamemwaga damu yao kama maji Pande zote za Yerusalemu, Wala hapakuwa na mtu wa kuwazika.


Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.


angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.


na Moabu atagaagaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?


kabla uovu wako haujafunuliwa bado, kama vile wakati ule walipokutukana binti za Shamu, na wale wote waliomzunguka, binti za Wafilisti wanaokudharau pande zote.


Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako;


Mwanadamu, Kwa sababu Tiro amesema juu ya Yerusalemu, Aha! Yeye amevunjika aliyekuwa lango la makabila ya watu; amenigeukia; nitajazwa kwa kuwa sasa ameharibika;


Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


basi tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu, naam, kwa sababu wamewafanya ninyi kuwa ukiwa, na kuwameza pande zote, mpate kuwa milki kwa mabaki ya mataifa, nanyi mmesemwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu;


Tena nitakufanya kuwa ukiwa, na aibu, kati ya mataifa wakuzungukao, machoni pa watu wote wapitao.


Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;


Wao hurudi, lakini si kwake Aliye Juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya ujeuri wa ndimi zao; na kwa sababu hiyo watachekwa katika nchi ya Misri.


Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.


Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.


Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo