Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ezekieli 23:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 watu wa Babeli, na Wakaldayo wote, Pekodi na Shoa na Koa, na Waashuri wote pamoja nao; vijana wa kutamanika, wote pia, watawala na mawaziri, wakuu, na watu wenye sifa, wote wenye kupanda farasi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Nitawachochea Wababuloni na Wakaldayo wote, watu toka Pekodi, Shoa na Koa, pamoja na Waashuru wote. Nitawachochea vijana wote wa kuvutia, wakuu wa mikoa, makamanda, maofisa na wanajeshi wote wakiwa wapandafarasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Nitawachochea Wababuloni na Wakaldayo wote, watu toka Pekodi, Shoa na Koa, pamoja na Waashuru wote. Nitawachochea vijana wote wa kuvutia, wakuu wa mikoa, makamanda, maofisa na wanajeshi wote wakiwa wapandafarasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Nitawachochea Wababuloni na Wakaldayo wote, watu toka Pekodi, Shoa na Koa, pamoja na Waashuru wote. Nitawachochea vijana wote wa kuvutia, wakuu wa mikoa, makamanda, maofisa na wanajeshi wote wakiwa wapandafarasi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Wababeli na Wakaldayo wote, watu kutoka Pekodi, na Shoa na Koa, wakiwa pamoja na Waashuru wote, vijana wazuri, wote wakiwa watawala na majemadari, maafisa wa magari ya vita na watu wa vyeo vya juu, wote wakiwa wamepanda farasi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Wababeli na Wakaldayo wote, watu kutoka Pekodi, na Shoa na Koa, wakiwa pamoja na Waashuru wote, vijana wazuri, wote wakiwa watawala na majemadari, maafisa wa magari ya vita na watu wa vyeo vya juu, wote wakiwa wamepanda farasi.

Tazama sura Nakili

Ezekieli 23:23
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.

Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.

Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.

wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa BWANA amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaelekee, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.

Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha ngome zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.

Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.

Neno la BWANA likanijia tena, kusema,

Aliwapendelea Waashuri, watawala na mawaziri, jirani zake, waliovikwa nguo za shani, wapanda farasi wakipanda farasi wao, wote pia vijana wa kutamanika.

Naye akaongeza uzinzi wake; kwa maana aliona wanaume, ambao sura zao zimeandikwa ukutani, sura za Wakaldayo zilizoandikwa kwa rangi nyekundu;

Kwa sababu hiyo, Ewe Oholiba, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawachochea wapenzi wako juu yako, hao ambao roho yako imefarakana nao, nami nitawaleta juu yako pande zote;

waliovikwa mavazi ya samawati, watawala na mawaziri, wote vijana wa kutamanika, wapanda farasi wakipanda farasi wao.

Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii mnayokaa ninyi sasa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo