Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 22:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Kama fedha iyeyushwavyo katika tanuri, ndivyo mtakavyoyeyushwa katikati mwake; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kama fedha iyeyushwavyo katika tanuri, ndivyo mtakavyoyeyushwa humo mjini. Nanyi mtatambua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nimeimwaga ghadhabu yangu juu yenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kama fedha iyeyushwavyo katika tanuri, ndivyo mtakavyoyeyushwa humo mjini. Nanyi mtatambua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nimeimwaga ghadhabu yangu juu yenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kama fedha iyeyushwavyo katika tanuri, ndivyo mtakavyoyeyushwa humo mjini. Nanyi mtatambua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nimeimwaga ghadhabu yangu juu yenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi bwana nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’ ”

Tazama sura Nakili




Ezekieli 22:22
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika, nitakuwa mfalme juu yenu;


Lakini waliniasi, wala hawakutaka kunisikiliza; hawakutupilia mbali kila mtu machukizo ya macho yake, wala hawakuviacha vinyago vya Misri; ndipo nikasema kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao, katikati ya nchi ya Misri.


Nawe utatiwa unajisi ndani ya nafsi yako, mbele ya macho ya mataifa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Naam, nitawakusanya, na kuwafukutia moto wa ghadhabu yangu, nanyi mtayeyushwa kati yake.


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.


Kwa hiyo nilimwaga hasira yangu juu yao, kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao.


Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga.


Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.


Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Nendeni mkayamwage yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo