Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 22:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Na mtu mmoja amefanya chukizo pamoja na mke wa jirani yake; na mtu mwingine amemharibu mke wa mwanawe kwa uasherati; na mtu mwingine ndani yako amemfanyia nguvu dada yake, binti ya babaye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Wengine hufanya machukizo kwa kulala na wake za majirani zao. Wengine hulala na wake za watoto wao, na wengine hulala na dada zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Wengine hufanya machukizo kwa kulala na wake za majirani zao. Wengine hulala na wake za watoto wao, na wengine hulala na dada zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Wengine hufanya machukizo kwa kulala na wake za majirani zao. Wengine hulala na wake za watoto wao, na wengine hulala na dada zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti ya baba yake hasa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti wa baba yake hasa.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 22:11
25 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na dada yake mzuri, aliyeitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.


Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, dada yangu.


Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye.


kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.


Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.


wala hakutenda mojawapo la mambo hayo yampasayo, bali amekula juu ya milima, na kumtia unajisi mke wa jirani yake,


hakula juu ya milima, wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakumkaribia mwanamke wakati wa kutengwa kwake;


Mnategemea upanga wenu, mnatenda machukizo, kila mmoja wenu anamnajisi mke wa jirani yake; je! Mtaimiliki nchi hii?


Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.


Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.


Mtu yeyote miongoni mwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA.


Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue.


Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.


Na mwanamume akilala na mkwewe mwanamke, wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo upotovu; damu yao itakuwa juu yao.


Tena mwanamume akimwoa dada yake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mwanamume; ni jambo la aibu; watengwa mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa dada yake; naye atauchukua uovu wake.


Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,


Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,


Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.


Na alaaniwe alalaye na dada yake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.


Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo