Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 21:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 “Ewe mtu, tabiri kuhusu Waamoni na maneno yao ya dhihaka kwa Waisraeli: Waambie kuwa nasema: Upanga, upanga! Upanga umenyoshwa kuua, umenolewa uangamize, umengarishwa ungae kama umeme.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 “Ewe mtu, tabiri kuhusu Waamoni na maneno yao ya dhihaka kwa Waisraeli: Waambie kuwa nasema: Upanga, upanga! Upanga umenyoshwa kuua, umenolewa uangamize, umengarishwa ungae kama umeme.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 “Ewe mtu, tabiri kuhusu Waamoni na maneno yao ya dhihaka kwa Waisraeli: Waambie kuwa nasema: Upanga, upanga! Upanga umenyoshwa kuua, umenolewa uangamize, umeng'arishwa ung'ae kama umeme.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 “Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu Waamoni na matukano yao: “ ‘Upanga, upanga, umefutwa kwa ajili ya kuua, umesuguliwa ili kuangamiza na unametameta kama miali ya radi!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 “Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao. “ ‘Upanga, upanga, umefutwa kwa ajili ya kuua, umesuguliwa ili kuangamiza na unametameta kama umeme wa radi!

Tazama sura Nakili




Ezekieli 21:28
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.


Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.


Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.


Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.


akawatwaa baadhi ya wazao wa kifalme; kisha akafanya agano naye, akamwapisha; akawaondoa watu wa nchi wenye nguvu;


Lakini alimwasi kwa kutuma wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! Atafanikiwa? Afanyaye mambo hayo ataokoka? Atalivunja agano, kisha akaokoka?


Utachora njia, ili upanga upate kufikia Raba wa wana wa Amoni, na kufikia Yuda katika Yerusalemu, wenye maboma.


wala sitakuacha usikie matusi ya wasioamini, wala hutaaibishwa na watu tena; wala hutalikwaza taifa lako tena, asema Bwana MUNGU.


Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo