Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 21:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ungae kama umeme, umengarishwa kwa ajili ya mauaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ungae kama umeme, umengarishwa kwa ajili ya mauaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kwa hiyo wamekufa moyo na wengi wanaanguka. Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote. Umefanywa ung'ae kama umeme, umeng'arishwa kwa ajili ya mauaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa mauaji kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama miali ya radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa kuchinja kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama umeme wa radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 21:15
15 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa.


Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.


Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa;


Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.


ukauambie msitu wa Negebu, Lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hadi kaskazini zitateketezwa kwa moto huo.


umenolewa ili kufanya machinjo; umesuguliwa ili uwe kama umeme; basi je! Tufanye furaha? Upanga unadharau fimbo ya mwanangu, kama unavyodharau kila mti.


Jiweke tayari, nenda upande wa kulia; jipange, nenda upande wa kushoto; mahali popote utakapouelekeza uso wako.


Tena, mwanadamu, ujiwekee njia mbili, upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja; hizo mbili zitatoka katika nchi moja; ukaandike mahali, upaandike penye kichwa cha njia iendayo mjini.


Katika mkono wake wa kulia alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.


Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;


Na itakuwa, wakuambiapo, Mbona unapiga kite? Ndipo utakaposema, Kwa sababu ya habari hizo, maana linakuja; na kila moyo utayeyuka, na mikono yote itakuwa dhaifu, na kila roho itazimia, na magoti yote yatageuka kuwa kama maji; tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU.


Na mara tuliposikia hayo mioyo yetu iliyeyuka, wala haukusalia ujasiri wowote katika mtu awaye yote, kwa sababu yenu; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu, katika mbingu juu na katika nchi chini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo