Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 16:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

45 Wewe u binti ya mama yako, amchukiaye mume wake na watoto wake; nawe u dada wa dada zako, waliowachukia waume zao na watoto wao; mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako Mwamori.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Kweli wewe ni mtoto wa mama aliyemchukia mumewe na watoto wake; wewe ni sawa na dada zako waliowachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Kweli wewe ni mtoto wa mama aliyemchukia mumewe na watoto wake; wewe ni sawa na dada zako waliowachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Kweli wewe ni mtoto wa mama aliyemchukia mumewe na watoto wake; wewe ni sawa na dada zako waliowachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Wewe ni binti halisi wa mama yako, ambaye alimdharau mume wake na watoto wake; tena wewe ni dada halisi wa dada zako, waliowadharau waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako alikuwa Mwamori.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Wewe ni binti halisi wa mama yako, ambaye alimchukia kabisa mume wake na watoto wake, tena wewe ni dada halisi wa dada zako, waliowachukia kabisa waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 16:45
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.


Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake.


useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.


Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.


Mwanadamu, palikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja;


Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.


Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.


Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.


Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo