Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 16:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

34 Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni tofauti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: Hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: Hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Katika umalaya wako hukufanya kama wanawake wengine: hakuna aliyekubembeleza ili uzini naye bali wewe ulilipa fedha badala ya kulipwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako. Hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, bali wewe ulikuwa tofauti kabisa, kwani ulilipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako, hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, wewe ndiye uliyelipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. Wewe ulikuwa tofauti.

Tazama sura Nakili




Ezekieli 16:34
5 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.


Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.


Watu huwapa makahaba wote zawadi, bali wewe unawapa wapenzi wako wote zawadi zako, na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote, kwa ajili ya mambo yako ya kikahaba.


Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la BWANA;


Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa porini aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo