Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ezekieli 13:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lolote!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Ole wenu manabii wapumbavu mnaofuata mawazo yenu wenyewe na maono yenu wenyewe!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Ole wenu manabii wapumbavu mnaofuata mawazo yenu wenyewe na maono yenu wenyewe!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Ole wenu manabii wapumbavu mnaofuata mawazo yenu wenyewe na maono yenu wenyewe!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote!

Tazama sura Nakili




Ezekieli 13:3
21 Marejeleo ya Msalaba  

Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.


Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.


Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.


BWANA wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha BWANA.


Kuhusu habari za manabii. Moyo wangu ndani yangu umevunjika, Mifupa yangu yote inatikisika. Nimekuwa kama mtu aliye mlevi, Na kama mtu aliyeshindwa na divai; kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.


Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawapa tumaini watu hawa kwa maneno ya uongo.


Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.


useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?


Ee Israeli, manabii wako wamekuwa kama mbweha, mahali palipo ukiwa.


Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?


Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.


BWANA akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu.


Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?


Ole wenu, enyi wanasheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.


Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!


amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matusi, na shuku mbaya;


Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao wanaume wawili ulivyokuwa dhahiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo