Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ezekieli 12:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema, Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 “Wewe mtu: Kwa nini methali hii inatajwa katika Israeli: ‘Siku zaja na kupita, lakini maono ya nabii hayatimii?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 “Wewe mtu: Kwa nini methali hii inatajwa katika Israeli: ‘Siku zaja na kupita, lakini maono ya nabii hayatimii?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 “Wewe mtu: Kwa nini methali hii inatajwa katika Israeli: ‘Siku zaja na kupita, lakini maono ya nabii hayatimii?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “Mwanadamu, ni ipi hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia’?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “Mwanadamu, ni nini hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia?’

Tazama sura Nakili




Ezekieli 12:22
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.


wasemao, Wakati wa kujenga nyumba hauko karibu; mji huu ni sufuria na sisi ni nyama.


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Mwanadamu, tazama, hao wa nyumba ya Israeli husema, Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana.


Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake.


Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari; nao watakwenda kwa nabii kutaka maono; lakini hiyo sheria itampotea kuhani, na mashauri yatawapotea wazee.


Ninyi mnaoiweka mbali siku hiyo mbaya, na kulileta karibu kao la udhalimu;


Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo