Ezekieli 11:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC1 Tena roho ikaniinua, ikanileta hadi katika lango la upande wa mashariki mwa nyumba ya BWANA, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema1 Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND1 Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza1 Roho ya Mungu ikaninyanyua na kunipeleka mpaka lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko nikawaona watu ishirini na watano wakiwamo Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, ambao ni viongozi wa Waisraeli. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu1 Ndipo Roho wa Mungu akaniinua na kunileta hadi kwenye lango la nyumba ya Mwenyezi Mungu linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango palikuwa na wanaume ishirini na watano. Nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu1 Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba ya bwana linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. Tazama sura |
Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.