Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Esta 9:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Esta 9:28
9 Marejeleo ya Msalaba  

Wayahudi wakaagiza na kutadaraki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili kulingana na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;

Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.

Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.

Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.

Na hayo mataji yatakuwa ya Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; yawe kumbukumbu katika hekalu la BWANA.

Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo