Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Esta 9:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Lakini Wayahudi wa Susa walikusanyika siku ya kumi na tatu ya mwezi huo, na siku ya kumi na nne pia; na siku ya kumi na tano ya mwezi uo huo wakapumzika, wakaifanya kuwa siku ya karamu na furaha.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini Wayahudi wa mji mkuu wa Susa walikusanyika pia siku ya kumi na nne lakini hawakupumzika. Waliadhimisha siku ya kumi na tano kwa furaha na shangwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini Wayahudi wa mji mkuu wa Susa walikusanyika pia siku ya kumi na nne lakini hawakupumzika. Waliadhimisha siku ya kumi na tano kwa furaha na shangwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini Wayahudi wa mji mkuu wa Susa walikusanyika pia siku ya kumi na nne lakini hawakupumzika. Waliadhimisha siku ya kumi na tano kwa furaha na shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

Tazama sura Nakili

Esta 9:18
7 Marejeleo ya Msalaba  

Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi katika kila mji wakusanyike na kuyalinda maisha yao, kwa kuangamiza, kuua, na kulimaliza jeshi lote la watu au mkoa watakaowashambulia, pamoja na watoto na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara;

Hata ulipofika mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, siku yake ya kumi na tatu, amri ya mfalme na mbiu yake ilipowadia kutekelezwa; ambayo siku ile adui za Wayahudi walitumaini kuwatawala, bali kumebadilika kinyume, hata Wayahudi waliwatawala wale waliowachukia;

Siku ile mfalme akaletewa hesabu ya hao waliouawa huko Susa mjini.

Ndipo Esta aliposema, Mfalme akiona vema, Wayahudi walioko Susa na wapewe ruhusa kufanya tena kesho sawasawa na mbiu ya leo, na hao wana kumi wa Hamani watundikwe juu ya mti ule.

Basi Wayahudi wa Susa wakakusanyika tena siku ya kumi na nne pia ya mwezi wa Adari, wakawaua watu mia tatu huko Susa; lakini juu ya nyara hawakuweka mikono.

siku ile ile Wayahudi wakakusanyika mijini mwao katika mikoa yote ya mfalme Ahasuero ili kuwatia mikono wale watu waliowatakia hasara; wala asiweze mtu kuwazuia, kwa kuwa waogopwa na watu wote.

kuwaonya wazishike siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na siku ya kumi na tano yake, kila mwaka,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo