Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Esta 8:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyanganya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyanganya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyang'anya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai asimamie shamba la Hamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani.

Tazama sura Nakili




Esta 8:2
11 Marejeleo ya Msalaba  

Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.


Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?


Ndipo mfalme alipoivua pete yake ya kupigia mhuri kutoka mkononi, akampa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.


Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi.


Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.


Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya utawala wote wa Babeli, na kuwa mtawala mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.


Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo