Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Esta 6:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lolote katika yote uliyoyasema.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.”

Tazama sura Nakili

Esta 6:10
7 Marejeleo ya Msalaba  

Jueni basi ya kwamba halianguki chini lolote la neno la BWANA, alilolinena BWANA juu ya nyumba ya Ahabu; kwa maana BWANA ameyafanya hayo aliyoyanena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya.

Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akampandisha juu ya farasi na kumtembeza kupitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.

na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa wakuu wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumpandisha juu ya farasi na kumtembeza kupitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.

Iweni hodari, na mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja BWANA.

Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.

Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo