Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Esta 4:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Pia akampa na nakala ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwoneshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.

Tazama sura Nakili




Esta 4:8
14 Marejeleo ya Msalaba  

Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye.


Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai.


Maana, ninawezaje kustahimili kuyaona mabaya yatakayowajia watu wangu? Au kuyatazama maangamizi ya jamaa zangu?


Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, siwezi kumjibu; Ni lazima nimwombe mshitaki wangu anihurumie.


Uombeeni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;


Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.


Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.


Naye Herode alikuwa amewakasirikia sana watu wa Tiro na Sidoni; wakamwendea kwa nia moja, na wakiisha kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulala, wakataka amani; kwa maana nchi yao ilipata riziki kwa nchi ya mfalme.


Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,


Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo