Esta 2:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC14 Huenda jioni, na asubuhi hurudi katika nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa awe amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema14 Jioni ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubuhi, mwali huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya Shaashgazi, towashi msimamizi wa masuria wa mfalme. Mwali haikumpasa kurudi kwa mfalme, isipokuwa kama mfalme amependezwa naye kiasi cha kuagiza aitwe kwa jina. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND14 Jioni ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubuhi, mwali huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya Shaashgazi, towashi msimamizi wa masuria wa mfalme. Mwali haikumpasa kurudi kwa mfalme, isipokuwa kama mfalme amependezwa naye kiasi cha kuagiza aitwe kwa jina. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza14 Jioni ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubuhi, mwali huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya Shaashgazi, towashi msimamizi wa masuria wa mfalme. Mwali haikumpasa kurudi kwa mfalme, isipokuwa kama mfalme amependezwa naye kiasi cha kuagiza aitwe kwa jina. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu14 Jioni angeenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme hadi apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu14 Jioni angekwenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme ambaye alikuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme mpaka apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake. Tazama sura |
Watumishi wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu yeyote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.