Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wakorintho 5:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwemo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Naam, tuna ujasiri, na tunaona ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana Isa.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.


Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.


Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.


Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;


Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.


Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.


Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.


Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.


Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.


Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumishi wake watamtumikia;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo