Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Mbali na mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa kila siku na mzigo wa wajibu wangu kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:28
12 Marejeleo ya Msalaba  

Baada ya siku kadhaa Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Turejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wako hali gani.


Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.


Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Ugiriki.


Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Nawiwa na Wagiriki na wasio Wagiriki, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima.


Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu,


ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao.


Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.


Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo