Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 9:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akamfitinia Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akapanga njama dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Waisraeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya shauri baya dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Israeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu,

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 9:14
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.


Na hao watu waliokuwako kambini wakasikia habari ya kwamba Zimri amekula njama, tena amemwua mfalme; kwa hiyo Israeli wote wakamfanya Omri, jemadari wa jeshi, awe mfalme juu ya Israeli siku ile kambini.


Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.


Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;


Mfalme wa Israeli akawaambia watumishi wake, Je! Hamjui ya kuwa Ramoth-Gileadi ni yetu? Nasi tumenyamaza tusiitwae mkononi mwa mfalme wa Shamu?


Ikawa asubuhi, akatoka, akasimama, akawaambia watu wote, Ninyi ni wenye haki; tazameni, mimi nalimfitinia bwana wangu, nikamwua; ila ni nani aliyewapiga hawa wote?


Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.


Na Hoshea mwana wa Ela akamfitinia Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.


Akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu ili kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu, huko Ramoth-gileadi; nao Washami wakamtia Yoramu jeraha.


Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli majeraha waliyotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.


Utakapofika huko, mtafute Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, ukaingie, ukamtoe miongoni mwa ndugu zake, ukamchukue katika chumba cha ndani.


Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo