Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 8:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Hazaeli akasema, Lakini mimi mtumwa wako ni nani, mimi niliye mbwa tu, hata nifanye jambo hili kubwa? Elisha akajibu, BWANA amenionesha ya kwamba wewe utakuwa mfalme juu ya Shamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hazaeli akauliza, “Lakini mimi mtumishi wako ni kitu kweli? Mimi niliye mbwa tu nitawezaje kutenda mambo hayo makubwa?” Elisha akamjibu, “Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba utakuwa mfalme wa Aramu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hazaeli akauliza, “Lakini mimi mtumishi wako ni kitu kweli? Mimi niliye mbwa tu nitawezaje kutenda mambo hayo makubwa?” Elisha akamjibu, “Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba utakuwa mfalme wa Aramu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hazaeli akauliza, “Lakini mimi mtumishi wako ni kitu kweli? Mimi niliye mbwa tu nitawezaje kutenda mambo hayo makubwa?” Elisha akamjibu, “Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba utakuwa mfalme wa Aramu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hazaeli akasema, “Itawezekanaje mtumishi wako, aliye mbwa tu, kufanya tendo la ajabu hivyo?” Al-Yasa akamjibu, “Mwenyezi Mungu amenionesha kuwa utakuwa mfalme wa Aramu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hazaeli akasema, “Itawezekanaje mtumishi wako, aliye mbwa tu, kufanya tendo la ajabu namna hiyo?” Al-Yasa akamjibu, “bwana amenionyesha kuwa utakuwa mfalme wa Aramu.”

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 8:13
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akasujudu, akasema, Mimi mtumishi wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi?


BWANA akamwambia, Nenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.


Na Hazaeli mfalme wa Shamu akawaonea Israeli siku zote za Yehoahazi.


Elisha akamwambia, Nenda, ukamwambie, Bila shaka utapona; lakini BWANA amenionesha ya kwamba bila shaka atakufa.


Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu.


Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa.


Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?


Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.


Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.


Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.


Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.


Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo