Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 6:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Na walipomteremkia Elisha akamwomba BWANA, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Adui waliposhuka kumwelekea, Al-Yasa akamwomba Mwenyezi Mungu: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Al-Yasa alivyoomba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wakati adui waliposhuka kumwelekea, Al-Yasa akamwomba bwana: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Al-Yasa alivyoomba.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 6:18
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakashindwa kuupata mlango.


Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria.


Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vile vile kama usiku.


Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.


Katika siku hiyo, asema BWANA, nitamtia kila farasi ushangao, na yeye ampandaye nitamtia wazimu; nami nitaifunulia nyumba ya Yuda macho yangu, nami nitamtia upofu kila farasi wa hayo makabila ya watu.


Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.


Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.


Basi, angalia, mkono wa Bwana uko juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.


Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.


BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo