Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 6:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mfalme wa Aramu akafadhaishwa sana na hali hiyo; akawaita maofisa wake, akawauliza, “Niambieni nani kati yenu anayetusaliti kwa mfalme wa Israeli?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mfalme wa Aramu akafadhaishwa sana na hali hiyo; akawaita maofisa wake, akawauliza, “Niambieni nani kati yenu anayetusaliti kwa mfalme wa Israeli?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mfalme wa Aramu akafadhaishwa sana na hali hiyo; akawaita maofisa wake, akawauliza, “Niambieni nani kati yenu anayetusaliti kwa mfalme wa Israeli?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Hili lilimfadhaisha sana mfalme wa Aramu. Akawaita maafisa wake, akawauliza, “Je, hamtaniambia ni nani miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Hili lilimfadhaisha sana mfalme wa Aramu. Akawaita maafisa wake, akawauliza, “Je, hamtaniambia ni nani miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?”

Tazama sura Nakili

2 Wafalme 6:11
8 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili.

Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.

hata ninyi nyote mkanifitinia, wala hapana mtu anifunuliaye habari hii mwanangu afanyapo agano na mwana wa Yese, wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia, wala kunifunulia ya kuwa mwanangu amemchochea mtumishi wangu, anivizie kama hivi leo?

Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli na alipoona kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimehatarisha uhai wangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo