Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 5:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Halafu Gehazi akaingia nyumbani kwa Elisha na kuanza kumhudumia. Elisha akamwuliza, “Ulikwenda wapi?” Gehazi akajibu, “Sikuenda mahali popote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Halafu Gehazi akaingia nyumbani kwa Elisha na kuanza kumhudumia. Elisha akamwuliza, “Ulikwenda wapi?” Gehazi akajibu, “Sikuenda mahali popote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Halafu Gehazi akaingia nyumbani kwa Elisha na kuanza kumhudumia. Elisha akamwuliza, “Ulikwenda wapi?” Gehazi akajibu, “Sikuenda mahali popote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Al-Yasa bwana wake. Al-Yasa akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?” Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakuenda popote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Al-Yasa bwana wake. Al-Yasa akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?” Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.”

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 5:25
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, na unakwenda wapi? Akanena, Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.


BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?


Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Wasemaje watu hawa? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, yaani Babeli.


Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.


Uzia akakasirika; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowakasirikia makuhani, ukoma ukamtokea katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa BWANA karibu na madhabahu ya kufukizia.


Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.


Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.


Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti.


Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;


Basi babaye mdogo akamwuliza Sauli na mtumishi wake, Je! Mlikwenda wapi? Naye akajibu, Tulikwenda ili kuwatafuta hao punda; na tulipoona ya kwamba hawakuonekana, tulimwendea Samweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo