Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wafalme 5:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Nabii akajibu, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, ninayemtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Nabii akajibu, “Hakika kama bwana aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 5:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;


Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.


Eliya akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo ambaye ninasimama mbele zake, hakika nitajionesha kwake leo.


Elisha akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe.


Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.


Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?


Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako baki nazo wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; lakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.


Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.


Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote.


Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo